February 28, 2021

 


ALIYEKUWA kocha msaidizi wa kikosi cha klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa kwa sasa yupo fiti kurejea ndani ya kikosi hicho, hii ni baada ya kufanyiwa upasuaji wa jino.

Mwezi mmoja uliopita, Mwambusi alitangaza kujiuzulu wadhifa wake ndani ya kikosi cha klabu ya Yanga, hii ni baada ya kushauriwa na daktari kutokana na kuwa na matatizo hayo ya kiafya ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Nizar Khalfan.

Akizungumzia maendeleo yake Mwambusi amesema: “Tayari nimepata matibabu ya jino, na ni kama wiki mbili zimepita tangu nifanyiwe upasuaji, naendelea vizuri na sina maumivu kama ilivyokuwa mwanzo.

“Wanamichezo waniombee nipone ili niweze kurejea katika majukumu yangu kama ilivyokuwa awali, na endapo nitakuwa sawa basi naweza kurejea Yanga”

 

 

 

 

 

 

9 COMMENTS:

  1. Aseme ukweli nini kilimtoa hapo na sasa anataka kurejea ktk nafasi ipi ili hali ilishajazwa?

    ReplyDelete
  2. Kweupe Kweupe nataka kumtowa Nizar tonge kinywani

    ReplyDelete
  3. Nizar haondoki... Karibu tena Mwambusi muda c mrefu utakuwa kocha mkuu

    ReplyDelete
  4. Ukweli timu imeyumba toka Mwambusi aondoke Yanga.Mwambushi ni mzuri Sana kwenye mbinu za kutafuta ushindi uwanjani.Timu inakuwa ina cheza kwa malengo kabisa.

    ReplyDelete
  5. Team has swayed badly since Mwambusi left the team.We need him back soon as possible.

    ReplyDelete
  6. Truly Yanga has swayed badly since Mwambusi left the team.We want him back to make our team strong tactically.

    ReplyDelete
  7. Yakale Ni dhahabu kumekucha kidimbwini, yetu NišŸ”„ wao tunaqatazamašŸ˜³šŸ˜³šŸ˜³wanatuchezaa movie

    ReplyDelete
  8. Na leo kwa Mkapa Mnyama atanguruma tena, tegeni masikio

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic