PRINCE Dube, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Azam FC amefanikiwa kutimiza majukumu yake kwa uzuri na kuipeleka timu hiyo hatua ya 16 bora Kombe la Shirikisho.
Bao lake la ushindi dakika ya 45+1, Uwanja wa Azam Complex limetosha kuwafungashia virago Mbuni FC ambao walikamilisha dakika 90 bila kuweka mzani sawa.
Ushindi huo wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina unaifanya Azam FC kuungana na Kagera Sugar, Simba, Yanga ambazo zimetinga hatua ya 16 bora.
Mchezo wake wa raundi ya tano watakutana na Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Hamsini Malale Uwanja wa Azam Complex.
Azam FC imeweka wazi kwamba malengo makubwa ni kupata ushindi kwenye mechi zao zilizobaki na kuweza kutwaa mataji ambayo wanayapambania.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema:"Malengo ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya kwenye mechi zetu ambazo tutacheza na kuweza kutwaa mataji,".
0 COMMENTS:
Post a Comment