February 23, 2021

 





FT: Simba 1-0 Al Ahly 

Uwanja wa Mkapa dakika 90 zimekamilika na Simba imeshinda mbele ya Al Ahly. Inafikisha pointi sita kwenye kundi A la Ligi ya Mabingwa na inaongoza kundi kwa sasa.

Bao la ushindi limefungwa na Luis Miquissone kiungo machachari na hatari akiwa na mpira ndani ya 18 ama nje ya 18.


Zinaongezwa dakika 4
Dakika 90 Manula anaokoa hatari baada ya mabekI kufanya uzembe na inakuwa on target ya kwanza
Dakika ya 89 Bwalya anapoteza mpira inachukuliwa na Al Ahly 
Dakika ya 86, Mugalu anatoka anaingia Kagere, anatoka Luis anaingia Kahata
Dakika ya 86 Luis anachezewa faulo anatolewa kwa machela
Dakika ya 85 Al Ahly wanafanya jaribio linapaa 
Dakika ya 83 Wawa  anaanua majalo
Dakika ya 82 Mugalu anaotea
Dakika ya 80, Tshabalala anachezewa faulo 
Dakika ya 79 Mugalu anaotea
Dakika ya 78, Manula anaokoa hatari
Dakika 1 ya kunywa maji
Dakika ya 74 Manula anaokoa hatari
Dakika ya 72 Mzamiru anafanya jaribio linakuwa kona
Dakika ya 71 Luis anasepa na kijiji cha watu wanne
Dakika ya 70 Nyoni anaingia Lwanga anatoka
Dakika ya 68, Lwanga anapewa huduma ya Kwanza 
Dakika ya 67 Al Ahly wanafanya jaribio halizai matunda
Dakika ya 64 Nyota wa Al Ahly anafanya jaribio linakwenda nje ya lango 
Dakika ya 61 Hamdi Fathi wa Al Ahly anapewa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Bwalya
Dakika ya 60 Luis anachezewa faulo 
Dakika ya 59 Mugalu anachezewa faulo na kipa mwamuzi anapeta
Dakika ya 56 Bwalya Walter Walter jaribio linaokolewa na Manula baada ya Luis kukosa faulo
Dakika ya 55 Kapombe anachezewa faulo nje kidogo ya 18
Dakika ya 53 Al Ahly wanalitafuta lango la Manula
Dakika ya 52 Mugalu anacheza faulo
Dakika ya 50 Wawa anamchezea faulo mchezaji wa Al Ahly 
Dakika ya 49 Mzamiru anaotea
Dakika ya 47 Lwanga anarudi uwanjani 
Dakika ya 46 Lwanga anachezewa faulo
Dakika Rarry Bwalya anaingia anatoka Dilunga 
Kipindi cha pili 
UWANJA wa Mkapa



Ligi ya Mabingwa Afrika,  hatua ya makundi

Mapumziko 

Simba 1-0 Al Ahly

Dakika ya 45 Kapombe anachezewa faulo 

Dakika ya 44 Al Ahly wanapata kona

Dakika ya 42 Manula anaokoa hatari

Dakika ya 40 Tshabalala anapiga shuti linakwenda nje kidogo ya lango

Dakika ya 39 Mugalu anafanya jaribio inakuwa kona

Dakika ya 38 Kapombe anafanya jaribio linaokolewa na mlinda mlango wa Al Ahly inakuwa kona

Dakika ya 37 Al Ahly wanapeleka mashambulizi Simba

Dakika ya 30 Goooooool Luis 

Dakika ya 28 Luis analazimisha kuingia na mpira ndani ya 18, Al Ahly wanaokoa

Dakika ya 26 Manula anaanzisha mashambulizi kwenda Al Ahly 

Mwamuzi anatoa dakika moja kwa ajili ya kunywa maji

Dakika ya 22, Bwalya Walter anapewa huduma ya kwanza

Dakika ya 20 Bwalya Walter anamchezea faulo Manula

Dakika ya 18 Simba wanaanzia nyuma kwa Tshabalala kuelekea mbele

Dakika ya 16 Al Ahly wanafanya jaribio linakwenda nje ya lango

Dakika ya 15 Luis anasepa nankijiji 

Dakika ya 14 Bwalya wa Al Ahly anamwaga maji lango la Manula, 

Dakika ya 13, Mugalu anaotea

Dakika ya 10 Mzamiru anapeleka mpira mbele unazuiwa na Al Ahly 

Dakika ya 8 mabeki wa Simba wanaruhusu moira uwapite, Manula anaokoa

Dakika ya 7 Al Ahly wanapata faulo nje kidogo ya 18

Dakika ya 5 Luis anachezewa faulo ndani ya 18

Dakika ya 3 Mugalu anapeleka mashambulizi Al Ahly 

Dakika ya 2 Manula anaqnzisha mashambulizi

11 COMMENTS:

  1. Asante Mnyama. Mulihifadhi goli hilo mupokee mamilioni yenu

    ReplyDelete
  2. Zisi izi Simba buana. Waarabu ulimi nje nje kudadadeki

    ReplyDelete
  3. Watasema na ikiwa bado hawajasema kuwa Mnyama kununuwa ushindi

    ReplyDelete
  4. Mimi ni Yanga lakini tuseme ukweli Simba inacheza vizuri sana hswa defensively: Onyango, Lwanga, na Wawa na Mzamiru wamenga'ra kwakweli kwa Simba hii sitashangaa wakifika Nusu Fainali CAF

    ReplyDelete
  5. Pongezi nyingi simba.Hii inadhirisha ubingwa wenu wa ligi kuu sio wa kubahatisha.

    ReplyDelete
  6. Kuna watu wamenuna wanasema Ahly kacheza chini ya kiwango ... Wataumia sana msimu huu

    ReplyDelete
  7. Almuradi sisi hatujafungwa na timu yoyote na mwaka huu ubingwa ni wetu sisi tena wa halali kwasababu sisi hatununui mechi

    ReplyDelete
  8. Viongozi wetu wa Yanga badala ya kujipanga kimkakati,kimipango,kiuchumi na kitaalam wamebaki kuitisha press conference kudai penalt na kumjadili Morrison,hawaoneshi weledi wala wana mikakati gani ya kupiga hatua.
    Kwa hakika roho inaniuma kuwapongeza Simba lakini sina budi kuwapa kongole maana kuna vitu vingine ukikataa kuvikubali basi utakuwa una chembechembe za husda na roho mbaya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utakuwa unaumia bila ya sababu.Hongera zako angalau Kwa kujitambua.

      Delete
  9. Kutokana na kiwango cha ajabu alichoonesha Mnyama jana wale wanaomchukia Mnyama walipigwa bumbuwazi na kutoa macho na hata ile zomea yao ya hapa na pale ilikuwa kama kitambaa kilichorowa maji na wakatoka nyuso chini wanangoja ubingwa wao wa kubabaishana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic