February 23, 2021


USIKU wa kuamkia leo picha ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba,(CEO), Senzo Mbatha akiwa na Kocha Mkuu wa Al Ahly ya Misri imezua gumzo kwa mashabiki wa Simba na Yanga ambao wamekuwa wakibishana kuhusu picha hiyo.

Miongoni mwa mashabiki wa Simba ambao walianzisha mdahalo kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na Agnes Daniel ambaye ni maarufu kwa jina la Miss Simba.

Miss Simba ameenda mbali kwa kusema kuwa ilipaswa Senzo ambaye kwa sasa yupo zake ndani ya Yanga akiwa ni Mshauri Mkuu kuelekea kwenye masuala ya mabadiliko alipaswa asubiri mpaka mechi ikiisha aonane na watu wa Al Ahly.


Kcezoo Machalan ambaye ni shabiki wa Yanga amesema kuwa ni muhimu Watanzania kuwa na subira kwa kuwa mtu kufahamiana na mtu sio uadui.

"Yaani Bongo mwana yaaani mtu akijuana na mtu basi ana majukumu, hayo mambo yaachwe kwa familia ya michezo,".

Leo Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi, Uwanja wa Mkapa.

8 COMMENTS:

  1. Ha!ha! Zahera alimpokea ibenge hawajashinda wife akiwa utopolo bado as Vita akafa hivyo Al shaky hatoki lazima afe kwa mkapa hakuna wakutosha wanaume

    ReplyDelete
  2. Waache wakutane, wote ni wasauthi inawezekana wanajuana

    ReplyDelete
  3. Wanajuana yaana waache utaifa wao kwasababu leo kuna mechi acheni ushabiki wa kizamani

    ReplyDelete
  4. Amina shida ya Nchi yetu hatutofautishi michezo na Vita na aliyemsindikiza picha Kama ni mwana habari hajatenda haki

    ReplyDelete
  5. Mwacheni ndio uwezo wake ulipoishia ndio mabadiliko anayowaandalia utopolo

    ReplyDelete
  6. Senzo kamsindikize nduguyo uwanja wandege na viazi wako wanaokusapoti.
    Sisi hatuangalii sura tunagonga tu.

    ReplyDelete
  7. Sezo vipi leo ameenda kumuaga airport? Shame

    ReplyDelete
  8. Huenda huko Al Ahli keshaoneshwa maslahi bora

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic