February 27, 2021



 LICHA ya kumaliza dakika 90 wakiwa pungufu, leo Februari 27, Uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Ken Gold bado waliweza kulinda ushindi wao wa bao 1-0 walilolipata.

Ni Fiston Abdulazack, ingizo jipya ndani ya Yanga ambaye alipachika bao la ushindi dakika ya 40 kwa mkwaju wa penalti uliomshinda kipa wa Ken Gold, Adam John.






Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha pili licha ya nyota wa Ken Gold kupambana kuweza kuweka usawa kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Jitihada zao zilikwama kwenye mikono ya kipa Faroukh Shikalo ambaye alianza kikosi cha kwanza.

Dakika ya 80 kiungo Carlos Carlinhos, raia wa Angola alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Ken Gold jambo lililopelekea mwamuzi kumuonyesha kadi hiyo.

Inakuwa ni kadi ya kwanza kwa nyota huyo wa Yanga mwenye mabao matatu ndani ya Ligi Kuu Bara na aliingia akitoka benchi kuchukua nafasi ya mshambuliaji Ditram Nchimbi.

Ushindi huo unaifanya Yanga itinge hatua ya 16 bora huku ikisubiri mshindi wa mchezo wa kesho kati ya Sahare All Stars ama Polisi Tanzania kwenye hatua ya 16 bora na timu hizo zinatarajiwa kumenyana kesho.

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa wachezaji walipambana kusaka ushindi na wamefanikiwa lengo lao jambo ambalo linawapasa pongezi.

7 COMMENTS:

  1. Sasa hiki kijamaa kutoka angola kinarusha ngumi ili hali hata nguvu hakina si kameambulia kadi ya bure tuu jamani?

    ReplyDelete
  2. Upambe mwingi kwenye uandishi, game haikuwa na ushindani hata kidogo. Tuseme tu ukweli ishu ya umaliziaji bado ni tatizo kwa Yanga.

    ReplyDelete
  3. kalinyoz,,

    Kamepiga ngumi ,,hii inamaana kamefuata maelekezo ya mwalimu kazehee ,

    ReplyDelete
  4. Duu mkwara wa kg 800 unafanya kazi refa angekataa ile penati na huku tungejitoa

    ReplyDelete
  5. Ijapokuwa wameshaelemewa na mambo Waelezwe na wafahamu kuwa huu si mchezo wa ngumi bali ni wa mpira unaojenga urafiki, mapenzi na kujuwana sio na nchi moja tu bali kote duniani na mpira umegeuka Biashara ambao umeshawafanya wengi duniani mamilionea na kuwa mpira sio uadui wa kupelekana mahakamani vituko ambayo mbona hatuvisikii kwengineko, labda huenda wakafahamu

    ReplyDelete
  6. Kutinga gani huko kwa peneti na kwa timu ndogo bado kukomaa kwa magumi na mateke, eti safari hii wanataka ubingwa wa kila pahala

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic