February 24, 2021


 BAADA ya Waarabu wa Misri Al Ahly kufungwa bao 1-0 mbele ya Simba kwenye mchezo wa  Ligi ya Mabingwa Afrika, Pitso Mosimane amesema kuwa hawajafungwa kwa mbinu bali hali ya hewa haikuwa rafiki kwao.

Bao la ushindi kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa lilipachikwa kimiani na Luis Miquissone dakika ya 30 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 jambo lililowamaliza wapinzani hao.

Mosimane amesema:"Tulikuwa tunajitahidi namna ya kwenda na wapinzani wetu na hili tulijua tangu awali jambo ambalo lilitufanya nasi tuongeze juhudi ndani ya uwanja.

"Kwa kilichotokea wanapaswa wapewe pongezi ila hatujapoteza kwa ajili ya mbinu zaidi ilikuwa ni hali ya hewa ambayo haikuwa rafiki kwetu.

"Muda wa jioni kwetu si rafiki hivyo tumejitahidi kwa namna ambavyo tumeweza tukashindwa kupata matokeo,hivyo mazingira hayakuwa rafiki kwetu, bado tuna kazi mbele na bado tuna mechi hivyo hatujakata tamaa,".

Mchezo huo ulichezwa majira ya saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Mara baada ya kukamilika kwa mchezo huo, Al Ahly hawakuwa na muda wa kubaki ndani ya ardhi ya Tanzania walikwea pipa na kurejea nchini Misri.


7 COMMENTS:

  1. Hali ya hewa ya jana mbona ilikuwa fresh tuu? Walitaka wacheze usiku ili waingize majini yao toka misri? Maana huo ndio utaratibu wao huko kwao.

    ReplyDelete
  2. Alitaka mbinu gani zaidi ya zilizotumika. Wao walionesha mbinu zipi? Angesema makosa ya kiufundi ningemwelewa.

    ReplyDelete
  3. Tumwulize wao walikosa magoli mangapi au kuna goli walifunga likakataliwaa?

    ReplyDelete
  4. Makanjanja hamjatunga hii stori nyie, maana hamuaminiki

    ReplyDelete
  5. 90 minutes 1 shoot on TARGET. SHAME ON YOU MOSIMANE, KAMA CAF WALIKUPA TUNZO YA KOCHA BORA WA AFRIKA WALIKOSEA BASI. HALI YA HEWA NDIYO ILIWAVUNJA MIGUU? UMEFANYA SUB 5 MPINZANI WAKO KAFANYA 4. UMETOA SAFU YOTE YA USHAMBULIAJI UKAWEKA MPYA. KWA HIYO WACHEZAJI WAKO WOTE WALIKUWA TATIZO NI HALI YA HEWA? BAYERN ALIWAFUNGA TATIZO HALI YA HEWA?

    ReplyDelete
  6. Asijidanganye hakuna timu kutoka misri ambayo ilishawah shinda Kwa mkapa, kawaulize wenzako

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic