WAKATI Yanga ikiwa inaongoza ligi, kocha mkuu wa timu hiyo, Mrundi, Cedric Kaze amekuwa akitumia kiasi cha shilingi milioni nane kwa siku 30 kulipa kodi katika nyumba anayoishi na familia yake.
Kaze amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Canada akitoka katika Akademi ya Barcelona ambapo ameiwezesha timu hiyo mpaka sasa kuchukua ubingwa wa Kombe la Mapinduzi huku wakiongoza Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 44 wakifuatiwa na Simba wenye pointi 35.
Kaze anayekunja mshahara wa dola 10,000 (Sh mil 23), analipiwa dola 120 (Sh 277,801) kwa ajili ya kulala tu.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga, kimesema kuwa, kocha huyo yeye ameamua kuishi kwenye apartment akiwa na familia yake ambapo kwa siku analipia dola 120 kwa ajili ya kulala pekee pale Palm Village Mikocheni jijini Dar karibu na mabosi wa Azam FC.
“Mwalimu yeye anaishi katika apartment ya Palm Village kwa sababu yupo na familia yake hapa nchini, kwa upande wa bei yake pale imechangamka kidogo.
"Pale halipii yeye bali uongozi ndiyo unalipia, kwa siku moja wanasema ni dola 120 ingawa tofauti huwa wanalipa kwa bili ya mwezi ambayo inafika milioni nane kwa kuwa familia yake bado inaishi pale licha ya mwalimu mwenyewe muda mwingi kuwa Avic Town inapokuwa timu wakati wote,” amesema mtoa taarifa.
Chanzo:Championi
Simba na Yanga wanatakiwa kuwa na nyumba zao binafsi kwa ajili ya wafanyakazi wao haswa wale wa benchi la ufundi: hii itazipunguzia timu hizi gharama zisizo kuwa na msingi.
ReplyDeleteDuh! Football is expensive
ReplyDeleteKwa vilabu vilivyo piga hatua wao kwa benchi la ufundi wanakodiwa nyumba za kuishi ama wanakuwa wamejenga zao? Tujifunze kwa hao wenzetu ili Tubadilike Mana garama kubwa zinatumika kwenye kodi ya nyumba.
ReplyDeleteHAO NI WATAKA SIFA, WAKATI UKIFIKA TUTAELEWA
DeleteAnaelipa uongozi au GSM?
ReplyDeleteWw si umeshaambiwa umbea wa nn au gsm yuko sehemu gan au hujui kia mdhamini naye kiongozi,,hujui kausha
DeleteInajulikana ni gsm
ReplyDeleteHAKUNA CHA AJABU MSHAHARA ANALIPWA DIEGO SIMEON BINGWA WA UEFA BAYERN AKIWA NA KOCHA HANS FLICK...MSHAHARA WA KAZE SIO KIGEZO CHA MAFANIKIO YA YANGA, HAYO MAPATANO YAO BINAFSI.
ReplyDeleteNashauri viongoz wa yanga na sisi tuandae mashindano yetu tuwalike ndanda na stend ...
ReplyDelete