February 1, 2021


 ALIYEWAHI kuwa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, anaripotiwa kuishitaki timu hiyo mahakamani.

Inadaiwa kuwa, Rweyemanu ambaye aliondolewa Simba mwaka jana baada ya Simba kupata matokeo mabaya mfululizo sasa inaripotiwa anataka kusafishwa na kulipwa fedha ambazo anaidai timu hiyo ili wamalizane vizuri.

Mechi mbili mfululizo Simba iliyeyusha pointi sita ilikuwa kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons na bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

 

Mwanasheria wake, John Feka, alikiri kuwepo kwa madai hayo ambayo yapo kwenye mahakama ya usuluhishi.

 

Feka amesema mteja wake ameitaka Simba kukanusha tuhuma zilizotolewa na timu ambazo zililenga kumchafua kwa makusudi.


 

“Kweli kesi ipo mahakama ya usuluhishi na kikubwa ipo kesi ya madai ya fedha ambazo ni siri.


“Kesi nyingine ya tuhuma ambazo amepewa mteja wangu zilitaka kumchamfua kutokana na tuhuma alizopewa,” alisema wakili huyo.


Chanzo:Championi

10 COMMENTS:

  1. HUYO SHIDA YAKE PESA TU, ATAPEWA YATAKWISHA ILA KAMA ANAJARIBU KULETA UKANJANJA IMEKULA KWAKE

    ReplyDelete
  2. Kwani kuna official taarifa iliyosema kuwa alikuwa anahunumu timu, au ananistukia tuu? Atulie huko simba hatakiwi tena baada ya kununuliwa na adui. ( not official info)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona na wewe unapita humo humo.....Una uhakika alinunuliwa?

      Delete
  3. Kama madai yake atalipwa ila kusafishwa asahau, yeye alikuwa mwajili hivi alifikiri Simba atakaa milele

    ReplyDelete
  4. Nguruwe fc lipeni hela yake mapovu yenu peleka chooni, jamaa anachotaka ni HELA tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Akili za nyani zipo kwenye makalio yake.Nyani fc masuala ya simba yanawahusu kweli?

      Delete
  5. Simba hawakukosea kumtimua huyu jamaa alikuwa anawahujumu na anachokifanya sasa ni muendelezo wa hujuma hizo.

    ReplyDelete
  6. Mlimlipa Vincent na Tambwe na Zahera?
    Manyani zama za Simba kudaiwa zilikwisha zamani. Hakuna wa kudai Simba kwa sasa. Inaendeshwa kitaalamu. Ndio maana hata makocha wakiondoka husikii wakidai.

    ReplyDelete
  7. Wekeni hadharani hujuma zake. Nyie akikosekana mchezaji mmoja tu mnafungwa halafu mnatafuta wa kumbebesha lawama.Tena jamaa mstaarabu, kadai chake tu angedai na ya kuchafuliwa jina je.

    ReplyDelete
  8. aje tulsafishe tumeandaa na mafuta kabisa ya kumpakaaaa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic