February 8, 2021

 



TIMU ya Taifa ya Morocco imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Chan ambao ulikuwa unashirikisha wachezaji wa ndani ya Bara la Afrika kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mali.

Mchezo huo wa fainali ulishuhudia kadi moja nyekundu katika dakika za lala salama ambapo nyota wa Mali Issaka Samake alionyeshwa kadi hiyo dakika ya 90+3.

Mabao ya Morocco ambao wamefanikiwa kutetea taji lao kwa mara ya pili yalifungwa na Soufiane Bouftini dakika ya 69 na bao la pili lilifungwa na Ayoub El Kaabi dakika ya 79, Uwanja wa Ahmadou Ahidjo, Cameroon.

Pia kwenye mashindano haya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilishia hatua ya makundi baada ya kukusanya pointi nne huku kwenye kundi lao ni timu ya Guinea na Zambia zilipenya hatua ya robo fainali.

Kutolewa mapema kwa Stars kulifanya wachezaji washuhudie fainali wakiwa kwenye ardhi ya Bongo kwa kuwa warirejea mapema Tanzania.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic