February 8, 2021


KOCHA wa Namungo FC, Hemed Morroco amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya 1 de Agosto ya Angola.

Namungo imetinga hatua ya 32 Kombe la Shirikisho ina kazi ya kufanya Februari 14, nchini Angola.

Jana, Februari 7 iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Majaliwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Morocco amesema kuwa anatambua utakuwa mchezo mgumu ila watapambana kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.

"Kila mchezaji anatambua kwamba tuna kazi ya kufanya kimataifa hivyo hilo linatufanya tuweze kuongeza nguvu kwa ajili ya mchezo wetu wa kimataifa.

"Makosa yetu ya kumalizia nafasi ambazo tunazipata tunayafanyia kazi hivyo ni muda wetu wa kuwa kwenye uimara na kufanya kwa umakini kusaka matokeo ndani ya uwanja," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic