February 3, 2021


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Yanga imefungiwa na FIFA kufanya usajili wa misimu mitatu kutokana na madai ya kutomlipa fedha za usajili pamoja na mshahara mchezaji wao wa zamani Amiss Tambwe.

 Kawaida FIFA hutoa adhabu kama hiyo kwa timu zilizoshindwa kutimiza agizo lake na hasa suala la malipo.

Habari za uhakika kabisa kutoka Zurich nchini Uswisi zinaeleza kuwa Yanga ilipewa siku 45 kumlipa mshambuliaji wake wa zamani Amissi Tambwe fedha anazowadai na muda huo ulishapita bila kulipwa.

Yanga bado hawajalipa hata senti kwa Tambwe ambaye anadai dola 19,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 43.7 na FIFA imewataka Yanga kuongeza asilimia 5 ikiwa kama ya usumbufu kwa mchezaji huyo.

Imeelezwa kuwa Tambwe anadai fedha hizo zikiwa za mishahara ya miezi miwili pamoja na kiasi kidogo ambacho hawakumlipa katika fedha yake ya Usajili.

11 COMMENTS:

  1. Hii havari ingekuwa inahusu simba nina hakika leo blog, magazeti, redio na tv zote ndio ingekuwa habari kuu. Hada wasafi na clouds

    ReplyDelete
  2. Hii habari ilikuwepo toka jana jan kwa sababu walipewa media day wakaacha kuandika kwa makusudi

    ReplyDelete
  3. NASIKIA HII NDIYO TIMU INAMLIPA MSHARA KAZE MILIONI 20 KWA MWEZI, KODI YA NYUMBA KWA MWEZI MILIONI 8, FISTON MSHAHARA WAKE UNALIPA MASTAA WA 3 WA SIMBA NADHANI ATAKUWA DUCHU, ALI SALIM, AU AME CJUI. LAKINI WAMESHINDWA KULIPA MILIONI 45 KWA MIAKA 3 HUKU TAJIRI YAO MUUZA NGUO ANASEMA WANA JAMBO LAO MWAKA HUU, WAKASEMA WALITOA MILIONI 300 KUWAPA WACHEZAJI BAADA YA KUPATA KOMBE LA UJI WA SEMBE.....SIJASEMA MIMI NI MEDIA ZIMERIPOTI.........POVU LUKSA

    ReplyDelete
    Replies
    1. We jamaaa kweli fikira zako ni ndogo kombe la uji wa sembe si ndo mlilianzisha nyie eti mkaita simpa inter cup kwa kuwaambia mtakao cheza nao wasiwafnge ila namshkuru mo aligundua mapema maana bila kakkombe hako sijui ka mngechukua nn mwaka huu.na mwishon mwa msim 2nasajiri kwa kishindo ili vibaraka wa mo muumie

      Delete
    2. Si tuliwatungua mikia aka paka mweusi

      Delete
  4. Yanga daima imekuwa ikissema ipo tayari na kwa thamani yoyote kutoa kwa ambae wanamhitaji, lakini wanashindwa kumlipa Tambwe masikini wa Mungu haki zake baada ya kuitumikia timu hiyo kwa misimu tafauti na kuipatia mafanikio makubwa. Hii ndio fadhila ya yanga ambayo kwa kila ukweli Simba hawanayo kwa sababu kila mwenye haki hulipwa haki yake kabla ya kukauka jasho lake na hii ndio siri kubwa ya mafanikio yao. Unaambiwa umlipe kibaruwa ajira yake kabla ya kukauka jasho lake

    ReplyDelete
  5. Lipeni deni huko. Mnawadanganya wachezaji eti mtawapa milioni 300, thubutu, yanga hii hii tunayoijua?

    ReplyDelete
  6. Aliwazalo mjinga hulipata.Mnawasingizia TFF na FIFA sijui mtasingizia nini!!!
    Utopolo kichwa cha panzi.
    Wenzenu wanaandaa mashindano wao wanawaita waandishi wawaangalie wakiogelea.
    Ujinga una asili.

    ReplyDelete
  7. Nyie Utpolo alias Vyura eleweni kuwa dawa ya deni ni kulipa.Mkiendelea na kiburi chenu basi msirudi kumtafuta mchawi kuwa ni TFF.Mna msururu wa madeni na kila mara wanaodai wanalia na kuwakumbushia na wengine wako kimyaa.Soon litafumuka la Chirwa, kocha Zahera,kocha Lwandamina,Anderw Vincent, kocha Luc Eyamel,Pondamali,

    ReplyDelete
  8. Saleh bwana, unapenda kutaka kuuza tu habari, WAMESEMA WATAWAFUNGIA MISIMU MITATU IKIWA HAWATAMLIPA TAMBWE, WE MWANDISHI WAWAPI UNADHANI HATUJUI

    ReplyDelete
  9. Clotus Chama aliona mbali sanaaaa, Yanga wababaishaji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic