February 28, 2021




 OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kuna kesi zaidi ya sita ambazo zitapelekwa mahakamani zikiwahusu watani zao wa jadi Yanga.

Hivi karibuni, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela aliweka hadharani kwamba wana mpango wa kumshitaki Manara ikiwa hataomba msamaha kwa kile alichoeleza kuwa aliharibu nembo ya timu hiyo kwa kuandika ujumbe usio na mantiki kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mkutano huo ulifanyika Februari 19,2021 mbele ya Waandishi wa Habari.



Ujumbe huo ulihusu jezi ya Yanga jambo ambalo Mwakalebela aliweka wazi kwamba lilishusha mauzo ya jezi. Kutokana na jambo hilo walitoa siku 14 ili aombe radhi na akishindwa kufanya hivyo watachukua hatua.

Manara amesema:"Siwezi kuomba msamaha kwa hilo hata nikipewa siku milioni, siwezi kwa jambo gani hasa, tena kesi kama hizo ninazipenda sana waache tu tuone itakuaje.

"Sasa nami ninasema kwamba hata wao tuna kesi nao, kuna kesi zaidi ya 6 zinawahusu tunaongea na mwanasheria wetu aweke mambo sawa hivi kunzia sasa na mambo yakikamilika kila kitu kitakuwa wazi.

"Zipo kama sita hivi ipo ya huyo Mwakalebela,(Fredrick) huyo Bumbuli,(Hassan Bumbuli) na wengine wengi hivyo wao wameanza nasi tunafuata hatuna mashaka tupo imara," amesema.

Bumbuli ni Ofisa Habari wa Yanga ambapo alifungiwa kujihusisha na soka kwa muda wa miaka mitatu na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) baada ya kukata rufaa amerejeshwa kazini rasmi.


8 COMMENTS:

  1. Sikuwa na taarifa kama Bumbuli alireheshwa kazini, mbona kama haikutangazwa?

    ReplyDelete
  2. Hapa ndo bongo mtu anatolewa kazini kwa kutangazwa lakini kuludishwa kazini sasa

    ReplyDelete
  3. Waswahili walinena" usimuamshe alielala, akiamka utalala wewe" Hapa ni kuwa alielala na kuamshwa ni Manara

    ReplyDelete
  4. Haina shida we peleka hizo kesi mahakamani sisi tutaanza kwa kufukua makaburi tujue zile kesi za utapeli ziliishia wapi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bingo! Na hii iliyoleta athari za kibiashara ina mashiko, itamtoa mtu kamasi!

      Delete
  5. Sio kola kesi ina mashiko, ndio maana kuna mahakimu, @Manara anajaribu kufanya diversity baada ya kuchafua brand ya watu, ndio anatishia Nyau Ili waogope lkn kesi zake hazina mashiko.
    Mfano: Senzo kukutana na mwananchi mwenzake wa South Africa eti nayo ni kesi kwa Manara.
    Sio mbaya apeleke mahakamani Ili mawakili wake wapate pesa za bure.

    ReplyDelete
  6. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic