FISTON Abdol Razack nyota mpya wa Yanga jana alifunga bao lake la kwanza ndani ya timu hiyo ambalo liliipa nafasi ya kusonga mbele hatua ya 16 bora kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho.
Bao hilo alipachika kwa penalti dakika ya 40 baada ya mpira kumfuata kwenye mkono nyota wa Ken Gold wakati Yanga walipokuwa wakifanya mashambulizi.
Jitihada za Yanga kuongeza bao la pili ndani ya dakika tano zilikwama baada ya Adam John, kipa wa Ken Gold kuwa kisiki kwa nyota wengi wa Yanga ambao walikuwa wakifanya majaribio kusaka ushindi.
Ni Fei Toto dakika 16 alipaisha mpira akiwa nje kidogo ya lango huku Fiston naye akionekana kukosa utulivu ndani ya eneo la 18.
Kipindi cha pili Ken Gold waliongeza juhudi kuweza kutafuta ushindi ila walikwama kumfunga Faroukh Shikalo ambaye aliweza kuokoa hatari.
Nyota Carlos Carlinhos alitumia dakika 14 ndani ya Uwanja wa Uhuru ambapo alifanya jaribio moja na kupiga kona mbili kabla ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kutokana na kitendo chake cha kumpiga ngumi mchezaji wa Ken Gold.
Hivyo atakosa mechi tatu zijazo ndani ya kikosi cha Yanga ambacho mchezo wake ujao ni wa ligi dhidi ya Coastal Union.
Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa ushindi ambao wameupata ni mwendelezo wa safari yao kuelekea yalipo malengo ya kutwaa taji la Kombe la Shirikisho.
Beki Boniface Mwanjonde wa Ken Gold ambaye alikutana na kitasa cha Carlinhos amesema kuwa jitihada zao zilikwama licha ya kupambana kusaka ushindi.
Ushindi huo unaifanya Yanga kusubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Sahare All Stars ama Tanzania Prisons ili wacheze naye hatua ya 16 bora.
He kumbe hii nayo ulimfuata mkono kama ile ya mbeya city
ReplyDelete