February 3, 2021


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes na msaidizi wake Seleman Matola, leo Februari 3 kimewasili salama makao makuu ya nchi Dodoma.

Jana, Februari 2 wachezaji walilipoti kambini baada ya kupewa mapumziko ya siku moja baada ya kukamilisha kusepa na taji la Simba Super Cup Januari 31, Uwanja wa Mkapa.

Simba ilitwaa taji hilo baada ya kukusanya pointi nne kwa kuwa ilishinda mchezo mmoja dhidi ya Al Hilal mabao 4-1 kisha ikalazimisha sare ya bila kufungana na TP Mazembe

Leo watakwenda pia bungeni kwa ajili ya kupewa baraka na Wabunge kuelekea kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Februari 12 kitacheza na AS Vita ya Congo.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi yao ya kesho pamoja na ile dhidi ya Azam FC.

"Tutapata nafasi ya kwenda pia bungeni kupata baraka kwa ajili ya kuiwakilisha nchi yetu kimataifa pia tuna kazi kubwa ya kusaka ushindi kwa mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji FC,".

Kesho Uwanja wa Jamhuri Dodoma kikosi cha Simba kitakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic