February 27, 2021


NYOTA wa Simba, Luis Miquissone mbali na TP Mazembe pamoja na Al Ahly kutajwa kuwania saini yake pia inaelezwa kuwa CD Belouizdad ya Algeria,Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, Al Hilal ya Sudan.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameweka wazi kwamba dau la mchezaji huyo sio la kitoto hivyo timu ambayo inahitaji kupata saini yake lazima ijipange.

"Uajua wengi wanauliza kuhusu Luis, yule ni aina ya wachezaji wa kipekee na wana uwezo mkubwa ndani ya uwanja hilo lipo wazi.

"Sasa tunajua kwamba kupitia mashindano haya ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa anachokifanya yeye pamoja na wachezaji wengine mawakala wanahitaji huduma yake sasa kumpata lazima zijipange kwa kweli.

"Naweka wazi kabisa dau la kumpata Luis kwa sasa ofa yake ya mwisho haiwezi kuwa chini ya Euro milioni moja hiyo ni ofa ya mwisho kabisa kwa mchezaji wetu.

"Dunia ya sasa inatumia Euro zaidi hivyo ofa yake haiwezi kuwa chini ya hiyo, nasema hivi hicho ni kiwango cha chini, kama Bwalya (Walter) kauzwa kwa dola milioni moja Al Ahly kwa nini Luis auzwe kwa chini ya kiwango hicho?

Nyota huyo amekuwa akitajwa kuwaniwa na timu nyingi kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja.

Mbele ya Al Ahly wakati Simba ikishinda bao 1-0 Uwanja wa Mkapa alitupia bao bora ambalo limezidi kumfanya awe gumzo.

Ikiwa kundi A inaongoza kundi na pointi zake ni sita, mechi zake mbili imeshinda zote ya kwanza ilikuwa ugenini dhidi ya AS Vita na ya pili mbele ya Al Ahly zote ilishinda bao mojamoja.

1 COMMENTS:

  1. Simba inatupiwa macho na timu nyingi nje na ndani ya bara la Africa hivi sasa hawa akina Dilunga na washikaji zake wazawa kama watajitoa fahamu kucheza kwa kujituma Kama Miqisone watatoka tu. Tatizo la vijana wetu wazawa nadhani wameanishwa Sana kuwa ikifika levo fulani basi wao hawawezi. Wanaweza Sana pengine kuliko Miqisone ila uoga umewazidi lakini wakati huu ndani ya simba ni wakati muafaka kwa wao kumshangaza hata kocha wao pale wanapopewa nafasi lakini vijana wetu wanakuwa kwenye kiwango Cha unyonge Sana kila pale wanapopata nafasi ya kuaminiwa na kocha.Nilifurahishwa na Ajibu kwenye FA cup zidi ya African Lyon na sitoshangaa kuona kocha akimpa shavu klabu bingwa Africa.Ila wakipewa nafasi na kocha wanatakiwa kuwa tayari kujitoa kwa timu na kubwa ni kwa wao wenyewe kujiongezea thamani kazini kupata maslahi bora zaidi.Kazi ya mpira ukiachana na kipaji lakini ujasiri wa mchezaji ndio unaotofautisha Kati ya mchezaji mwenye malengo na yule anaecheza kwa mazoea. Kapombe Manula wapo vizuri kwenye levo ya Africa kabisa. Shabalala ni very talented player ila wakati mwengine huwa anapoteza umakini kiulaini sana katika tackling. Beki tatu au mbili kiuhalisia ni sawa na mchezaji wa mwisho wa kumlinda kipa anatakiwa kuwa makini mno katika kukaba licha ya kuwa na kazi ya kuanzisha mashambulizi pia.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic