DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba amesema kuwa mchezo wake ujao dhidi ya Al Merrikh utakuwa mgumu tofauti na wengi wanavyofikiria.
Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Simba ikiwa ipo kundi A ipo nafasi ya kwanza na ina pointi sita, mechi zake zote mbili imeshinda.
Ilianza kushinda ugenini mbele ya AS Vita 0-1 Simba kisha ikashinda bao 1-0 dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Mkapa.
Mchezo wake unaofuata wa Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa Machi 6, ugenini nchini Sudani, timu hiyo ilikuwa mikononi mwa Gomes kabla ya kuibukia ndani ya Simba Januari 24 kuchukua mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye yupo zake Morocco.
Gomes amesema:"Kuhusu hilo tuna muda mwingi wa kufikiria juu ya mechi ijayo, itakuwa mechi ngumu kwa sababu naijua hiyo timu. Lakini kwa sasa nadhani tunatakiwa kutojipa mawazo sana kuhusiana na mechi hiyo inayokuja.
"Wachezaji wanajua kwamba tunahitaji ushindi ila inahitaji muda na tutapambana ili kupata matokeo chanya ndani ya uwanja, kikubwa sapoti pamoja na umakini kwani kuna kazi kubwa ya kufanya,".
Yeye anaijua merreck, na merreck wanamjua yeye. Hapo pagumu
ReplyDeleteKweli itakuwa ngumu wachezaji wa al merrekh wanafahamu mbinu zake vzr kwahyo inaweza kuwa ngumu kwa simba ukifananisha na alvocheza na al ahly na as vita walijipigia tu
ReplyDeleteWatakufa tu, simba sc home and away safi tu
ReplyDeleteMlisema alipochoze na alhaly. Sasa mmekuwa washabik wa al merekh.
DeleteNaamini tutapata point 3 au 4 game zote mbili.
ReplyDeleteUtopolo mtuache na team yetu
ReplyDeleteMungu awatangulie tu kwa kila stage
ReplyDeleteAsalam Aleykum! All games is big game! So we need big saport from all arier cz Simba is not perfect in away.Mingu ibariki Tanzania na uibariki Simba Kwa uwezo wako c ujanja wao
ReplyDelete