February 15, 2021

 


Anaandika Antonio Nugaz, Ofisa Uhamasishaji wa Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze:- 

Mwanachama na shabiki wa Yanga, kwanini ukajikosesha amani kwa timu kutoka sare na kuaminishwa kuwa timu haitopata matokeo na wewe unaamini hilo.

Kumbuka mpaka sasa tuko kileleni (namba moja) kwenye msimamo wa ligi na pia tukiwa na rekodi sahihi ya kutopoteza mchezo hata mmoja.

Lazima tukubaliane na matokeo ya mpira na sio kulaumu sana kana kwamba tuko nafasi ya 8 au tunaburuza mkia.

Tambeni mtaani, msitembee kinyonge, vimbeni mtaani na muendelee kuipa hamasa timu yetu Insha Allah kila kitu kitaenda sawa.

Kisha tukutane Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumatano kwenye mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar saa 1:00 usiku tujitokeze kwa wingi bila kukosa.



6 COMMENTS:

  1. Tutambe vipi wakati kilamtu ansjua juzi tulibebwa. Sisi mashabiki wenu tuna khofu sasa ikiwa mipango yenu ya kurubuni wachezaji na marefa sasa kwenye mzunguko wa pili haifanyi kazi tena labda hamuwalipi wanaotufanyia madili

    ReplyDelete
  2. Mashabiki wenyewe wanajua kama wanastahili kutamba ama la, wala sio suala la kuhamasisha

    ReplyDelete
  3. Tutambe nini nasi tunawekewa vizingiti na kila aina ya mazengwe na wale wenye hela yao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mara tu yamekuwa hayo nyie si ndo mlikuwa mnasema Mo mpaka wakae kikao Cha familia Ela ndo itoke, mda si mrefu utasikia TFF ni Simba

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic