MESHACK Abraham, mshambuliaji wa kikosi cha Gwambina FC anatajwa kuwekwa kwenye rada za mabosi wa Yanga ili kuweza kuona uwezo wake kwenye mechi za ushindani.
Nyota huyo ambaye jina lake limetajwa na Kocha Mkuu, wa timu ya Taifa ya Tanzania, Kim Poulsen kwenye orodha ya wachezaji watakaongia kambini Machi 8 kujiandaa na mechi za kufuzu Afcon alikuwa kwenye hesabu za kutua kikosini hapo ila dili lake likabuma.
Kwa sasa Yanga inapambana kurejea kwenye ubora huku ikiwa imekosa washambuliaji wenye uwezo wa kuwa na mwendelezo mzuri ndani ya uwanja, ambapo kwenye mechi 21 imefunga jumla ya mabao 34 na kinara ni winga Deus Kaseke mwenye mabao 6.
Michael Sarpong na Yacouba Songne ambao ni washambuliaji hawa wametupia mabao manne kila mmoja huku nyota Ditram Nchimbi akiwa ametengeneza pasi mbili za mabao.
Habari kutoka ndani ya Gwambina zimeeleza kuwa Yanga wanampigia hesabu nyota huyo.
"Yanga inahitaji huduma ya Abrahm ila kwa sasa itakuwa ngumu kwa kuwa dirisha la usajili limefungwa hapo itakuwa ni mpango ujao na kwa sasa wanachokifanya ni kumfuatilia kwenye kila mechi ambazo anacheza," ilieleza taarifa hiyo.
Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa tatizo lipo kwenye umaliziaji wa nafasi ambazo wanazitengeneza jambo ambalo atalifanyia kazi.
Ndani ya Gwambina FC, Abraham ametupia jumla ya mabao 7.
Mnachukuwa wachezaji munaowaita mitambo ya magoli lakini mkishawapta wanayeyuka na baada wa muda wanafika fifa kudai haki zao
ReplyDeleteUkiwa unajaribu tena na tena na matokeo ni yale yale ya kufeli ni dalili ya uendawazimu.Huwezi ukabadilisha 1+1 ikawa 3.Hata urudie mara ngapi.
ReplyDeleteUkiona mbinu unazotumia zinafeli na wewe unarudia minuter zile zile ujue ukichaa upo karibu.