DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba alimbadilishia majukumu beki wake wa kati, Kenedy Juma kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Mkapa kwa kumpa mikoba ya Shomari Kapombe.
Keneddy ambaye aliibuka ndani ya Simba akitokea Singida United ni miongoni mwa mabeki ambao jina lake lipo kwenye orodha ya nyota walioitwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Juzi wakati African Lyon 0-3 Simba, alipewa mikoba ya kumwaga maji ambapo alionekana akiimudu kazi hiyo huku akitumia nguvu kubwa kuwazuia nyota wa African Sports kupita upande wake.
Gomes amesema kuwa lengo la kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake ni kuweza kuwapa nafasi wale ambao hawachezi mara kwa mara pamoja na kuwapa mapumziko wachezaji wengine.
Ni African Lyon, sio African Sports.
ReplyDeleteafrican sport imeandikwa wapi
ReplyDeleteInaonesha una makengeza pacha wewe...kila mtu ameona mahali palipoandikwa African Sports halafu wewe unabisha
DeleteImeandikwa African Sports, acha ubishi. African Sports ni ile iliyoichapa Yanga juzi juzi, wakati African Lyon ni ile iliyochapwa na Simba juzi hapo
DeleteAnabisha facts mpe pole
DeleteSoma uelewe, African sports imetajwa, usibishe kabla ya kujiridhisha
ReplyDeleteJuzi wakati African Lyon 0-3 Simba, alipewa mikoba ya kumwaga maji ambapo alionekana akiimudu kazi hiyo huku akitumia nguvu kubwa kuwazuia nyota wa African Sports kupita upande wake.
ReplyDeleteakitumia nguvu kubwa kuwazuia nyota wa African Sports kupita upande wake.
ReplyDelete