IMEELEZWA kuwa Klabu ya Liverpool ipo kwenye mpango wa kuachana na kocha wao Jurgen Klopp katika nafasi hiyo kutokana na kuamini kwamba anaweza kupata dili la kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani.
Jina la Steven Gerrad linatajwa kuwa kwenye orodha ya makocha ambao wanapewa nafasi ya kuchukua mikoba ya Klopp ambaye anapambana kutetea taji la Ligi Kuu England ambalo alitwaa msimu uliopita.
Pia kuna mashaka kuwa huenda Klopp akapewa kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani ambayo ipo mikononi mwa Joachim Low.
Habari zinaelezwa kuwa Klopp anatazamwa kwa ukaribu na chama cha soka cha Ujerumani, (DFP) na wana mpango wa kufanya naye mazungumzo hivi karibuni ili aweze kuibuka ndani ya timu ya taifa.
Low amefanya kazi na timu ya taifa ya Ujerumani kwa muda wa miaka 15 na 2014 aliweza kukiongoza kikosi hicho kutwaa Kombe la Dunia ila hakuweza kutetea taji hilo 2018 hivyo anahitaji kujiweka kando akihofia kufutwa kazi jumlajumla.
0 COMMENTS:
Post a Comment