March 2, 2021


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa hali ya kipa namba moja wa timu hiyo Aishi Manula kwa sasa ipo sawa baada ya jana kugongana na mchezaji wa JKT Tanzania, Daniel Lyanga.

Manula aliumia dakika ya 67 baada ya kugongana na Lyanga akiwania mpira ndani ya uwanja ambapo wachezaji wote wawili waliumia ila Manula ilikuwa zaidi kwa kuwa alipoteza pia fahamu.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ameongea na Manula na amemwambia kwamba yupo sawa isipokuwa anaskia maumivu kwa mbali.

"Aliwahishwa hospitali ya Kairuki na alipewa matibabu na kurejea kwenye hali yake ya kawaida kwa kuwa baada ya kupoteza fahamu aliweza kurejewa na fahamu muda mfupi akiwa ndani ya Ambulace.

"Yassin Gembe, daktari wa Simba ambaye alikuwa na Manula ameniambia kwamba yupo sawa na anaendelea vizuri hivyo anaweza kuelekea Sudan kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Al Merrikh ambapo kikosi kinatarajiwa kuondoka kesho.

"Leo ataruhusiwa na atapewa mapumziko kabla ya kesho kuungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya kujiunga na kikosi kitakachoelekea nchini Sudan,". 

Simba itamenyana na Al Merrikh ya Sudan kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi Machi 6.

7 COMMENTS:

  1. Asante Mungu, maana Aishi Manula ndiyo tegemeo kubwa. Ikiwa angeshindwa kupona ingekuwa hasara kwa timu, kusaifiri na makipa wawili inaweza kutokea la kutokea.

    ReplyDelete
  2. Tuliathirika nae sote na tunamuomba Mungu Muweza amuondoshee maumivu ambayo nasi pia tumeyahisi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic