March 2, 2021


IMERIPOTIWA kwamba Klabu ya Liverpool inawania saini ya kiungo wa Klabu ya Udinesse, Rodrigo De Paul ili ajiunge ndani ya kikosi hicho cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England.

Mbali na Liverpool kuwania saini ya nyota huyo raia wa Argentina ambaye anacheza ndani ya  Serie A pia Klabu ya Inter Milan nayo inatajwa kuwania saini ya kiungo huyo.

Akiwa na miaka 26 anaonekana kuwa bora ndani ya uwanja jambo ambalo limewafanya Liverpool wavutiwe naye na wapo tayari kuweka mkwanja mezani ili kupata saini yake.

Dau ambalo Liverpool inatajwa wameweka ni Euro milioni 30 kupata saini ya nyota huyo ambaye kwa msimu huu wa 2020/21 amecheza jumla ya mechi 23 amefunga mabao matano na pasi tatu za mabao na kwa upande wa kadi ameonyeshwa kadi mbili za njano na moja nyekundu.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic