March 4, 2021


 

BEKI wa kati wa Simba, Joash Onyango amesema kuwa baada ya mechi tatu kupita ndani ya Simba atarudisha muonekano wake wa zamani wa ndevu nyeupe ambao alikuwa nao.

Onyango raia wa Kenya ni ingizo jipya ndani ya Simba aliibuka huko akitokea Klabu ya Gor Mahia huko alikuwa na muonekano wa nywele nyeupe zilizokuwa zikimfanya awe na muonekano wa mchezaji mzee.

Umri wake wa miaka 28 umekuwa ukizua gumzo kwa mashabiki kutokana na umbo lake jambo lililowafanya wengi wabeze usajili wake ila kwa anachokifanya kwa sasa wameanza kukaa kimya taratibu.

Kwenye Ligi Kuu Bara, Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 19 za ligi na kufunga mabao 45 yeye amefunga bao moja pia ni chaguo la kwanza kwa Didier Gomes ambaye ni Kocha Mkuu wa timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa hatua ya makundi.

Alifunga bao hilo kwenye mchezo wake wa kwanza wa dabi mbele ya Yanga kwa kichwa akimalizia kona iliyopigwa na Luis Miquissone. Bao la Yanga lilifungwa na Michael Sarpong kwa mkwaju wa penalti baada ya mwamuzi wa kati kutafsiri kwamba Onyango alimchezea faulo Tuisila Kisinda.

Onyango amesema:”Kwa sasa nina mpango wa kurejesha muonekano wangu ule wa zamani. Zile ndevu zangu nyeupe zitarudi ila ni baada ya mechi tatu hivi nitaweza kurejea kwenye ule muonekano wangu wa zamani.

"Kwa kufanya hivyo itakuwa zawadi kwa wale wajukuu zangu ambao wanapenda kuniita mzee na nimezikumbuka kweli hivyo ninaweza kuzirejesha," .

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic