March 2, 2021


 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union ameweka wazi kuwa kwa sasa wanaowaza kwamba timu hiyo itashuka daraja wasahau jambo hilo kwa kuwa bado wana mechi mkononi.

Coastal Union yenye maskani yake Tanga imekuwa kwenye mwendo wa kusuasua msimu wa 2020/21 ambapo kwenye msimamo ipo nafasi ya 13 ikiwa imekusanya pointi 23 baada ya kucheza mechi 21.

Mchezo wake wa ligi unaofuata ni dhidi ya vinara wa ligi, Yanga wenye pointi 49 unaotarajiwa kuchezwa Machi 4 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ambapo kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa Yanga ilishinda mabao 3-0.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa wana mechi zaidi ya 15 mkononi jambo ambalo litawafanya wapambane kupata matokeo chanya.

“Hakuna habari ya kushuka kwa sasa na ikiwa nitazungumza kwamba nitashuka sitakuwa sawa, ukitazama kuna mechi zaidi ya 15 mkononi za kucheza na ligi inaendelea sasa hapo unadhani nitafikiria kuhusu kushuka?  Hapana kabisa hatushuki tutapambana,”.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic