March 26, 2021


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Barcelona ina mpango wa kuwauza wachezaji wake wanne ili waweze kupata mkwanja kwa ajili ya kulipa madeni ambayo wanadaiwa.

Kwa mujibu wa El Confidencial, timu hiyo inadaiwa mkwanja mrefu kutokana na janga la Virusi vya Corona ambalo limefanya mapato wa timu nyingi duniani kushuka kwa sababu hakukuwa na mashabiki ambao wanaruhusiwa kuingia uwanjani pamoja na shughuli za kiuchumi nyingi kusimama.

Majina ya wachezaji hao wanne ambao wamewekwa sokoni ni pamoja na Antonio Griezmann, Coutinho, Samuel Umtiti na Francisco Trincao.

Coutinho ambaye alijiunga na Klabu ya Barca akitokea Liverpool msimu wa 2018 kwa dau la pauni milioni 142 amecheza jumla ya mechi 90 na ametupia mabao 24, Griezmann bado hajawa kwenye ubora baada ya kuibuka ndani ya Camp Nou akitokea Klabu ya Atletico Madrid.

Janga la Corona limetibua mipango mingi ya timu duniani hasa kwenye uchumi na ilipeleka kupunguza mishahara ya wachezaji ndani ya Barcelona ili kuweza kupata nguvu ya kumudu gharama.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic