March 1, 2021

 


DENZIL Mkandla, meneja wa wachezaji wa Klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe amesema kuwa mpango mkubwa wa kwanza katika usajili ni kupata saini ya Luis Miquissone anayekipiga ndani ya Simba.


Mkandla ameweka wazi kuwa Luis ni mchezaji wa kipekee ndani ya uwanja kwa kuwa anaonyesha kiwango cha hali ya juu muda wote.


FC Platinum ilitolewa na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kukubali kichapo cha mabao 4-0 Uwanja wa Mkapa ila ule mchezo wa Kwanza, Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ilishinda bao 1-0.


Mfungaji wa bao la FC Platinum,  Perfect Chikwende kwa sasa yupo ndani ya Simba akiwa ni maalumu kwa michezo ya ndani ambapo ameshaanza kucheza mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Mkandla amesema:"Sisi tuna wachezaji wazuri na wanafanya kazi nzuri ndani ya uwanja, ila kwa pale Simba mchezaji ambaye ni chaguo letu la kwanza kumpa dili ni Luis kwani ana uwezo na kasi,".

1 COMMENTS:

  1. Kama kweli wanayo hela ya kumnunuwa Luis ilikuwaaje wakashindwa kumzuwia Chikwende, mchezaji ambae nyota kwao aliyewapatia goli moja. Ni fujo tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic