LEO Machi 16, Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba atakiongoza kikosi chake kusaka pointi tatu mbele ya Al Merrikh ya Sudan kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Al Hilal, ubao ulisoma Al Merrikh 0-0 Simba hivyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Wakati Simba ikiingia Uwanja wa Mkapa bila ya mashabiki pia Gomes atakosa huduma ya beki kisiki Pascal Wawa ambaye ana kadi mbili za njano pamoja na kiungo mkabaji Thadeo Lwanga.
Gomes ameweka wazi kuwa bado ana wachezaji wengi ambao anao na anaamini kwamba watafanya vizuri kwenye mchezo wa leo.
"Ukiangalia kwa upande wa beki wa kati yupo Peter Muduhwa ambaye ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa, anaweza kucheza pia beki wa kati kwa kuwa amekuwa na uelewano mkubwa na Wawa pamoja na Joash Onyango.
"Katika eneo hilo pia yupo Kenedy Juma, Ibrahim Ame hawa wanaweza kufanya kazi hiyo kwa ukamilifu.
"Kwa upande wa kiungo mkabaji ninaweza kubadili mfumo lakini kwenye mechi iliyopita alicheza Mkude, (Jonas) yupo pia Erasto Nyoni hivyo bado kuna namna ya kufanya," amesema.
Huyo Muduhwa hatujawahi kumwona, lakini kwa kuwa kocha anasimamia mazoezi yeye ndio anajua. Nyoni na Mkude wanafahamika
ReplyDeleteAachiwe mwenyewe kocha kukipanga kikosi chake cha Misimba dume kumi na moja kingurume kwa uhuru
ReplyDeleteHata akipigwa pia kipigo kimwendee yeye asiwepo wa kuhoji
ReplyDeleteKENEDY WILSON JUMA CHAGUA LA KWANZA. PETER MUDWA NI MASHINE BALAA. HUYU AMELETWA KUMRITHI WAWA KIAINA ILA WALIO WENGI HATUJUI. LUKOSA AMELETWA KUMRITHI KAGERE KIAINA
ReplyDelete