March 23, 2021


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa mchezo wao dhidi ya AS Vita utakuwa na ushindani mkubwa jambo ambalo analitambua na amewaambia wachezaji wake.

Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ipo hatua ya makundi inaongoza kundi A na pointi zake 10 ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya AS Vita, Aprili 3 Uwanja wa Mkapa.

AS Vita kwenye kundi A ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 4 inahitaji kufufua matumaini ya kusonga mbele na kutinga hatua ya makundi kama ilivyo kwa Simba jambo ambalo litaongeza ugumu kwenye mchezo huo.

Gomes amesema:"Nimewaambia wachezaji kwamba haitakuwa kazi nyepesi kwetu na kila timu inahitaji ushindi hivyo ni muhimu kujipanga vizuri.

"Ikiwa tutashindwa kupata matokeo itakuwa ngumu kwetu kufikia malengo ya hatua ya robo fainali hivyo tupo tayari kufanya vizuri," .

1 COMMENTS:

  1. uyu kocha ananishangazaga kwenye hzi mechi Molirson ndio wakutupa matokeo yeye anadili na Chama na Mugalu tu duuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic