March 25, 2021


KUFUATIA taarifa za kupata majeraha akiwa ndani ya kikosi cha Taifa Stars, Beki wa klabu ya Yanga, Dickson Job ameibuka na kuwatoa hofu mashabiki wake hususani waajiri wake klabu ya Yanga, kwa kusema kwa sasa anaendelea vizuri.

Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Mtibwa Sugar hajaichezea Yanga mchezo wowote tangu ajiunge nao Januari mwaka huu.

Hii ni baada ya kupata majeraha ya misuli aliyoyapata akiwa ndani ya kikosi cha Stars, kilichokuwa kikijiandaa na michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Akizungumzia maendeleo yake, Job alisema: “Ni kweli nilipata majeraha madogo wakati wa maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya Equatorila Guinea.

“Hii ni kutokana na kurejea kutoka majeruhi hivyo sikuwa sawa kiutimamu wa mwili, hivyo nilishauriwa kupata mapumziko kidogo, lakini kwa sasa naendelea vizuri,”

 

2 COMMENTS:

  1. Huyu dogo toka amesajiliwa anapata Misukosuko sana, sijui hatma yake itakuwaje? Atapimwa kwa kigezo gani kama hachezi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic