March 25, 2021


TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeweka wazi kuwa maandalizi yote ya mchezo wao wa leo dhidi ya Equatorial Guinea yamekamilika, kilichobaki ni wao kupambana uwanjani ili kusepa na pointi tatu ugenini.

Leo Alhamisi majira ya saa 4:00 usiku, Taifa Stars itakuwa Nuevo Estadio de Malabo kupambana na Equatorial Guinea katika mchezo wa tano wa Kundi J.

Katika kundi hilo, Taifa Stars inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne, baada ya kucheza michezo minne. Vinara wa kundi hilo ni Tunisia wenye pointi 10, wakifuatiwa na Equatorial Guinea wenye pointi sita, huku Libya wakiburuza mkia na pointi tatu.

Meneja wa Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema: “Tumekuwa na maandalizi ya muda mrefu kuanzia nyumbani Tanzania na kumalizia Kenya ambapo tulipata nafasi ya kucheza mchezo wa kujipima nguvu, hivyo ni matarajio yetu kuwa maandalizi hayo yatatupa matokeo mazuri,"

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen, amesema: “Naridhishwa na kiwango cha utayari wa vijana wangu, tunakwenda kucheza mchezo huu tukijua wazi kuwa hatuko kwenye nafasi nzuri, lakini nafasi bado tunayo na tutapambana kufanikisha ndoto hiyo," 

Naye nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, amesema: “Nina imani mechi itakuwa ngumu, lakini kwetu itakuwa mechi yetu ya fainali na wao wanalifahamu hilo.

“Equatorial Guinea wanacheza nyumbani, watataka kutumia kila ambacho wanaweza kupata ushindi, sisi tumejiandaa vizuri kusaka ushindi.

“Mwalimu amekuwa na timu kwa wiki mbili na maandalizi ni mazuri. Mchezo huu ndiyo utatupa nafasi ya kushiriki AFCON kwa mara nyingine,"


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic