March 26, 2021

 


KATIKA kuhakikisha kikosi chake kinakuwa imara katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi ameongeza program ya mazoezi ya gym.

 

Yanga imepanga kufanya vema msimu huu ikiwemo kubeba makombe yote wanayoshindania ikiwemo ligi na FA ambayo yote yanatetewa na Simba.

 

Program hiyo ya gym ambayo Yanga wameianza ndiyo inayotumiwa hivi sasa na Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes katika kukisuka kikosi chake kinachoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Spoti Xtra, lina taarifa za kambi ya Yanga iliyopo Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Dar es Salaam chini ya Mwambusi ambaye ameongeza program ya mazoezi katika kuwaweka fiti nyota wake.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata gazeti hili, Mwambusi ameongeza program hiyo wanayoifanya asubuhi, huku jioni wakifanya mazoezi ya kimbinu uwanjani.

 

“Timu tangu imerejea kambini mara baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu Kaze (Cedric) aondolewe imekuwa ikifanya mazoezi kwa program moja pekee ya uwanjani saa kumi jioni.

 

"Lakini kocha Mwambusi tangu alipopewa timu alianza na mazoezi ya kuchezea mpira na kukimbia mbio fupi na ndefu muda wa jioni na hiyo ni katika kutengeneza fitinesi ya wachezaji.

 

“Lakini juzi walipoingia tena kambini, kocha ameongeza program ya gym itakayokuwa inafanyika kila siku asubuhi.


 “Jioni kocha amepanga kuwapa program ya kuchezea mpira ikiwemo mazoezi ya kimbinu ya jinsi ya kufunga na kulinda goli wakati timu ikiwa imepoteza mpira,” alisema bosi mwenye cheo kikubwa Yanga.

 

Alipoulizwa Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Yanga, Hassani Bumbuli, kuzungumzia hilo, alisema: “Kama uongozi kila kitu kinachohusiana na ufundi tumemuachia kocha na sisi viongozi tunasimamia masuala ya kiutawala, kuhusu maandalizi ya timu yanakwenda vizuri katika kujiandaa na michezo ijayo," .


Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kambini ni pamoja na Michael Sarpong, Faroukh Shikhalo.

4 COMMENTS:

  1. Mkichukua kocha Mfaransa nasi pia tunachukuwa kama huyo lakini ikiwa ila kwa bei powa na kila aina ya mazoezi anayowapa wachezaji wake nasi kama hayo, anaondoka mguu wake nasi tunaweka mguu wetu Mpaka kijulikane tunalotaka kuzoa makombe yetu

    ReplyDelete
  2. Pia tafuteni msemaji mwenye kiwango cha Haji Manara

    ReplyDelete
  3. Mmeamini Simba ni next level kwani tulipoleta kocha mbelgiji utopolo wakaiga sasa hivi tuna mfaransa nao wanataka kuiga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic