March 26, 2021


 IMEELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Azam FC, Ally Niyonzima huenda atawekwa kando msimu ujao kutokana na kushindwa kufiti mipango ya mabosi hao wa Dar.

Niyonzima ambaye ni ingizo jipyakutoka Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda alijiunga na timu hiyo kwenye usajili wa dirisha kubwa.

Habari zimeeleza kuwa Kocha Mkuu wa Azam FC amewaomba mabosi wa timu hiyo kumtafuta kiungo mwingine jambo ambalo linaashiria kuwa safari ya kiungo huyo imefika tamati.

"Kocha anahitaji kupata kiungo mkabaji mwingine kwani bado huyu ambaye yupo bado hajaweza kufiti hivyo atakayesajiliwa atakuwa katika ubora," ilieleza taarifa hiyo.

Hivi karibuni Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit alisema kuwa kuhusu usajili wa timu hiyo wanachotazama ni ripoti ya ya kocha.

2 COMMENTS:

  1. Huyo kwanza Alitakiwa na yanga na walikuwa wakimsifu kupindukia kiasi na angelikuja wakati ule angepokekewa kwa mbwembwe nyingi kule airpot kama alivopokekewa Kaze na wengineo a wengi wao kwa sasa wameshatimuliwa

    ReplyDelete
  2. Habari ni Azam nashangaa kwenye comment atajwa yanga kwahiyo humuwezi kupumua bila ya kuitaja yanga??

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic