March 22, 2021




 UONGOZI wa Ruvu Shooting umeweka wazi kuwa kwa mshambuliaji wao matata Fully Zully Maganga kukabwa na beki wa Klabu ya Manchester United, Harry Maguire itakuwa dharau kubwa.

Maneno hayo yamewekwa wazi ikiwa ni muda mfupi baada ya Klabu ya Manchester United kupoteana kwenye mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Leicester City.

United ikiwa na beki wake ghali, Maguire ilikubali kichapo cha maba 3-1 jambo ambalo limewaondoa kwenye reli United na harakati za kutimiza lengo la kutwaa taji la FA.

Kupitia ukurasa wao wa Twiter, Ruvu Shooting waliadika namna hii:"Fully Zullu Maganga akabwe na Mwagwaya, (Maguire) kweli si dharau hizi,".

Maguire mwenyewe amesema:"Tulikuwa tunahitaji ushindi ila tumekosa hakuna wa kumlaumu kwa wakati huu na hakuna namna ya kufanya zaidi ya kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo,".

Ilikuwa ni Uwanja wa King Power mchezo wa robo fainali Kombe la FA.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic