BAADA ya mshambuliaji wa bora wa muda wote ndani ya Klabu ya Manchester City, Sergio Arguero kuripotiwa kwamba anaodoka ndani ya kikosi hicho msimu huu mkataba wake utakapoisha, Klabu ya Manchester United inapewa nafasi ya kupata saini yake.
Arguero ndani ya Etihad ameshamalizana na mabosi wake na kupitia kikao ambacho walikaa pamoja na Kocha Mkuu wa timu hiyo Pep Guardiola na mabosi wa timu hiyo iliwapa nafasi mabosi wake kutangaza kwamba hatakuwa pamoja nao msimu ujao.
City waliweka wazi Machi 29 kwamba hawatakuwa na nyota huyo ambaye amedumu kikosini hapo kwa muda wa misimu 10 akiwa na rekodi ya kucheka na nyavu mara 257 katika michuano yote na mkataba wake unameguka Juni, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Foot Mercato imeripoti kwamba raia huyo wa Argentina ana ofa nyingi mkononi ikiwa ni pamoja na ile ya kutoka kwa Manchester United.
0 COMMENTS:
Post a Comment