SAFU ya ushambuliaji ya Mtibwa Sugar inayoundwa na Kelvin Sabato inampasua kichwa kocha wao Hitimana Thiery kwa kuwa inashika rekodi ya kuwa safu namba moja kwa ubutu Bongo.
Kwenye
Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar ikiwa imecheza jumla ya mechi 22, imefunga mabao 9
na safu yake ya ulinzi imeokota jumla ya mabao 16.
Ikiwa
ipo nafasi ya 14 na pointi zake 24 haijawa na mwendo mzuri jambo ambalo
lilimfaya Zuber Katwila kubwaga manyanga na sasa yupo zake ndani ya Ihefu FC.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Hitimana amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na
watapambana kurejea kwenye hali yao ligi itakapoendelea.
“Ni
kweli hatujawa kwenye mwendo mzuri, ila jambo la msingi ni kuweza kufanya maandalizi
mazuri na kupambana kwa wakati ujao kupata kwa matokeo, ili upate matokeo ni
lazima timu ifunge hilo lipo wazi tutalifanyia kazi,” amesema.
Safu ya
Simba inaongoza kwa kufunga mabao mengi ikiwa imefunga jumla ya mabao 46 na
imecheza mechi 20.







0 COMMENTS:
Post a Comment