KIKOSI cha klabu ya soka ya Namungo kesho Jumapili kinatarajia kuanza rasmi mazoezi ya kujiwinda na mchezo wao wa tatu wa makundi kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Ijumaa ya Aprili 2.
Namungo inakamatia nafasi ya tatu kwenye msimamo
wa kundi D la michuano hiyo ikiwa bado haijapata alama yoyote.
Pyramids na Raja Casablanca ndiyo vinara wa msimamo na pointi
zao sita, huku Nkana wao wakiwa wanabuluza mkia baada ya kufungwa michezo yao
miwili kwa idadi kubwa ya mabao kulinganisha na Namungo.
Akizungumzia mipango yao, Ofisa habari wa klabu ya Namungo Kindamba Namlia amesema: “Kikosi chetu
kinatarajia kuanza rasmi mazoezi kesho Jumapili, kwa ajili ya mchezo wetu ujao wa
kombe la Shirikisho dhidi ya Nkana utakaochezwa Aprili 2, mwaka
huu,"
0 COMMENTS:
Post a Comment