March 22, 2021


 ADAM Adam, nyota wa timu ya JKT Tanzania ambaye anacheza ndani ya Klabu ya JKT Tanzania amesema kuwa malengo yake makubwa msimu huu ni kufunga mabao mengi zaidi ili kuipa mafanikio timu yake.

Adam ni mzawa wa kwanza msimu wa 2020/21 kufunga hat trick ambapo aliwatungua Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex.

Timu yake inapambana kusaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi kutokana na mwendo wake kutokuwa mzuri kwa msimu wa 2020/21.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 23 imekusanya pointi 24 ipo nafasi ya 14. Imeshinda mechi 6 na imepoteza mechi 11 na kulazimisha sare 6. Ikiwa imefunga mabao 22 yeye amefunga mabao 7.

Adam amesema:"Ninapenda kufunga mabao mengi ndani ya timu yangu ya JKT Tanzania na ikiwa itakuwa hivyo itakuwa ni faida kwa timu kwa kuwa nitapata muda wa kutimiza majukumu yangu na tutabaki ndani ya ligi.

"Ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi ila haitufanyi tukate tamaa katika mechi zetu mapambano ni lazima yaendelee," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Apambane sana na kuongeza fiziki yake yupo nyoronyoro sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic