March 2, 2021


 IKIWA kesho inatarajiwa kuanza safari kuelekea nchini Sudan kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi dhidi ya Al Merrikh, nyota wake 9 mikataba yao inatarajiwa kumeguka msimu utakapoisha.

Simba chini ya Didier Gomes ambaye ni Kocha Mkuu, inakazi ya kusaka ushindi ndani ya kundi A ambapo kwa sasa inaongoza ikiwa na pointi sita baada ya kukusanya pointi hizo kwenye mechi zake mbili.

Hawa hapa nyota hao ambao mikataba yao inaweza kumeguka msimu ukikamilika ndani ya ligi 2020/21:-  Nahodha msaidizi, Mohamed Hussein `Tshabalala' kiungo mkabaji Jonas Mkude nahodha John Bocco.

Kipa namba mbili, Beno Kakolanya kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib beki wa pembeni Shomari Kapombe na Gadiel Michael.

Pia kiungo Francis Kahata wengi wanapenda kumuita kijiko na kiungo mshambuliaji Miraji Athumani.

Kuhusu wachezaji kundoka ndani ya Simba, hivi karibuni Ofisa Habari wa Simba Haji Manara alisema kuwa mpango wa Simba ni kuwa na wachezaji makini na haitaweza kumuachia mchezaji yeyote ambaye anatakiwa ndani ya kikosi hicho kinachotetea taji la Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

7 COMMENTS:

  1. Hii taarifa unaileta hapa leo ili iweje, nanusa harufu ya uchokozi. Acha simba watulize akili zao kwa mechi ngumu wanayoiendea wewe utakuwa umetumwa au umejituma kuvuruga mambo, ushindwe.

    ReplyDelete
  2. We jamaa, uto wako unakuumiza. Pole sana.habari za Chama zimekushinda umegeukia lingine. Hahaaa.

    Wasaidie Uto kushusha pressure waliyonayo Kwa sasa. Utopolo

    ReplyDelete
  3. Ni kweli, ni kuwa inahusu nini na kwa fhamira gani kuyaleta haya wakati huu ambapo timu ipo katika. Juu muandishi anakusudia udalali kujuulisha timu nyengine kujiweka tayari kuwa huku wachezaji au kuwafanya wachezaji ambao wamo katika hekaheka kubwa ya kutafuta ubingwa wababaike. Kwa namna timu ilivo na wachezaji walivokinai hapana ataebabaika kwasababu wanaojuwa vizuri wanayoyapsta huku hawatoyapata kwengine kokote

    ReplyDelete
  4. Utopolo nendeni mkale utopolo wenu tuacheni na Simba yetu itupe laaha yaaani no kukonda ni mwendo wa kunenepa tu

    ReplyDelete
  5. Washamba sana hawa jamaaa.inawahusu nn.maisha ya mtu

    ReplyDelete
  6. UNADHANI NANI ATAWEZA KUWASAJILI?

    ReplyDelete
  7. Kwanini msizungumzie mambo ya msingi mnazungumzia upuuzi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic