MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania
amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kumaliza ndani ya tano bora kwa
msimu wa 2020/21.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 23 imekusanya
pointi 30 ipo nafasi ya 9 na kinara ni Yanga mwenye pointi 50 baada ya kucheza
mechi 23 huku nafasi ya tano ikiwa mikononi mwa KMC yenye pointi 35.
Akizungumza na Spoti Xtra, Malale alisema kuwa
mpango mkubwa wa timu hiyo ni kumaliza ndani ya tano bora jambo ambalo
linawezekana.
“Bado tuna mechi za kucheza na hesabu zetu ni
kuona kwamba tunamaliza kwenye msimamo tukiwa ndani ya tano bora ili tupate
nguvu ya kuanza vizuri msimu ujao.
“Kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wangu mwanzo
mwa msimu ilifanya tuanze kwa kusuasua ila kwa sasa hawa ambao wamekuja wameipa
nguvu timu na tunazidi kupambana kupata matokeo,” alisema Malale.







0 COMMENTS:
Post a Comment