SUD Abdi Mohamed, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania amesema kwamba ni jukumu la kila mwamuzi kutumia weledi wake wote kazi katika kutimiza majukumu yake.
Kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara
kumekuwa na matukio ya wachezaji kuonekana wakiwalalamikia waamuzi kutokana na
kutoridhishwa na maamuzi yao.
Pia wachezaji nao wamekuwa wakifanya makosa ambayo yanawafanya waamuzi wawaadhibu kwa kuwaonyesha kadi na wakati mwingine kwa kuzungumza nao ili wasiweze kurudia makosa hayo.
Mohamed amesema kuwa wamekuwa wakiwapa mafunzo waamuzi ili waweze kutimiza majukumu yao kwa weledi jambo ambalo wanatakiwa kulifanya muda wote.
“Waamuzi wote wamekuwa wakipewa mafunzo kila
wakati hasa pale ligi inapoanza na tumekuwa tukikumbushana umuhimu wa kutimiza
majukumu kwa kufuata sheria na ikiwa watafanya hivyo wataepuka makosa ambayo
yanatokea.







0 COMMENTS:
Post a Comment