March 26, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amesema kuwa kufariki kwa Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli ni mipango ya Mungu kwa kuwa alimuita na akaitika.

Samia ameyasema hayo kwenye ibada maalumu ya kumuaga Magufuli ambayo imefanyika kwenye kanisa maalumu lililojengwa Uwanja wa Magufuli, Chato Geita leo Machi 26. Magufuli ambaye alitangulia mbele za haki Machi 17 kwa maradhi ya moyo anatarajiwa kupumzishwa Chato, Geita.

“Tumempoteza kiongozi wetu shujaa, mpenda amani na mchapakazi. Mungu alimuita naye ameitika hivyo kazi yetu ni lazima tufanye kwa heshima na kwa unyenyekevu ili kuyaenzi yale ambayo aliyatenda.

“Kuondoka kwake ni pigo lakini bado tutaendelea kusimama na hatutayumbishwa katika utendaji wetu. Sikuwahi kufikiria kwamba ningekuja hapa kumsindikiza pale ambapo aliwahi kunionyesha kwamba huwa wanawapumzisha ndugu zao.



"Hakuna namna ya kufanya zaidi ya kuendelea kushikamana, kuwa wamoja na kufanya kwa umakini," amesema.  

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic