March 26, 2021


 GWIJI wa Real Madrid, Fernando Hierro amesema kuwa anatarajia kumuona nyota wa kikosi hicho Sergio Ramos akiongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Hierro amesema kuwa anaamini kwamba beki huyo  ataongeza mkataba ambao utakuwa ni wa kuitumikia timu hiyo maisha yake yote.

Mkataba wa Ramos ndani ya kikosi cha Real Madrid unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa msimu huu na mpaka sasa ishu ya mkataba wake mpya mambo bado ni magumu.

"Ninapenda kumuona Sergio Ramos akiendelea kuichezea Real Madrid na kustaafia hapo kwani ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic