March 19, 2021

HATIMAYE kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Burundi, Saidi Ntibazonkiza 'Saido' ameanza mazoezi rasmi mara baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili.

Mara ya mwisho Ntibazonkiza kuonekana Uwanjani ilikuwa Januari 13 mwaka huu, katika mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba uliofanyika Visiwani Zanzibar.

Ntibazonkiza ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya nyonga tayari ameanza mazoezi katika kikosi cha timu ya taifa ya Burundi, ambacho  kinajiandaa na michezo ya kufuzu kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya timu ya taifa ya Afrika ya kati unaotarajiwa kufanyika Machi 26 mwaka huu.

Kiungo huyo amekuwa mhimili mkubwa kwa timu hiyo kwani tayari alifanikiwa kuifungia timu hiyo mabao 2 na kutoa pasi 3 za mabao katika michezo ya ligi kuu.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Burundi Olivier Niyungeko alithibitisha kurejea kwa nyota huyo katika kikosi cha timu ya taifa hilo, huku akisema kuwa hali ya mchezaji huyo imeimarika ila hajafahamu kama atamtumia katika mchezo unaofuata wa timu hiyo.

“Ntibazonkiza amerejea na tayari yupo katika kikosi chetu anaendelea vizuri na mazoezi, kuhusu kumtumia katika mchezo wetu ujao dhidi ya Afrika ya Kati.

"Bado sijajua kwani kama unavyofahamu mchezaji akitokea katika majeruhi anahitaji muda mzuri wa kukaa sawa,” amesema kocha huyo.

 

 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic