March 6, 2021


 Shabiki wa Klabu ya Simba na Liverpool, Joel Mtalamu ameshinda Sh 78,265, 530  baada ya kubashiriki kwa usahihi zaidi matokeo ya michezo 12 ya mpira wa miguu ya ligi mbalimbali duniani kupitia droo ya Perfect 12.

Mtalamu ambaye ni mkazi wa Kidatu, Kilombero anakuwa mshindi wa nane wa droo hiyo tokea kuanza kwa mwaka huu kwa mujibu wa Meneja  wa Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi.

Mushi amesema kuwa wanajisikia fahari kubwa sana kuendelea kuwainua vipato Watanzania kupitia michezo yao ya kubahatisha. Washindi hao wanaingia katika orodha yao ya nyumba ya mabingwa.

“Ni faraja kwetu kuona Watanzania wengi wanashinda kupitia michezo yetu ya kubahatisha.   Tutaendelea kuwa nyumba ya mabingwa huku tukiendelea  kuwainua vipato vyao,” amesema Mushi.

Kwa upande wake, Mtalamu aliipongeza kampuni hiyo kwa kufanya shughuli zake kwa uwazi na kuwazawadia washindi. “Nimefarijika sana kushinda, hizi fedha nitaanzisha biashara mpya huku nikihimarisha biashara yangu,” amesema Mtalamu.

Wakati huo huo jumla ya washindi wanne wameshinda zawadi ya fedha katika mchezo mpya wa kubahatisha wa M-Bet unaotambulika kwa jina la Shinda Extra.

Washindi hao ni  Daniel Mbasha,  Hamisi , Victor na  Jusiri Allem ambao kila mmoja amejishindia Sh500,000.

Kupitia mchezo huo, M-Bet itakuwa inatoa zawadi ya Sh500,000 kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa na Sh.milioni 1 kwa siku za Jumamosi na Jumapili.

Mushi amesema kuwa kampuni hiyo itatumia si chini ya Sh18 millioni kuzawadia washindi kupitia mchezo huo. Alisema kuwa kwa wachezaji ambao wamejisajili kupitia app ya M-Bet  watalipa Sh500 ambapo hawajasajiliwa watalipa sh.1000.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic