March 4, 2021


UONGOZI wa Simba umesema kuwa sababu kubwa za nyota wake watano kuachwa kwenye ardhi ya Tanzania ni mipango ya Kocha Mkuu Didier Gomes mwenyewe kutokana na sababu mbalimbali.

Jana Machi 3, kikosi cha Simba kilikewea pipa na jumla ya wachezaji  25 kuwafuata wapinzani wao Al Merrikh kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi unaotarajiwa kuchezwa Machi 6.

Nyota waliobaki Bongo ni pamoja na mshambuliaji mpya Junior Lokosa, kiungo mshambuliaji Bernard Morrison, beki wa kati Ibrahim Ame.

Pia yupo kiungo mkabaji Said Ndemla  pamoja na kiungo mshambuliaji Perfect Chikwende ambaye ni ingizo jipya pia kutoka FC Platinum.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa yote ni mipango ya kocha kwa kuwa ameamua kuondoka na wachezaji 25 hivyo hakuna tatizo lolote.

"Mwalimu ameona hawa wachezaji 25 ni sawa hivyo ambao wameachwa kuna sababu ambazo zipo, kwa mfano yupo Chikwende,(Perfect) huyo hata kwenye orodha ya wachezaji wa mechi za kimataifa hayupo.

"Kikubwa ni kuona namna gani kikosi na wachezaji watapambana kwa ajili ya kusaka ushindi ndani ya uwanja,".

Kwenye kundi A Simba inaongoza kundi ikiwa na pointi sita ina kazi ngumu ya kusaka ushindi mbele ya Al Merrikh ambayo haijaonja ushindi kwenye mechi zake mbili za Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi.

5 COMMENTS:

  1. Kipindi hiki cha COVID 19 ni vema kwenda na wachezaji wote wanaostahili kucheza maana huwezi jua vipimo vya COVID vitatokaje. Kuacha wachezaji bila sababu ya msingi ni hatari zaidi

    ReplyDelete
  2. Inauma bora kungekuwa na sababu za msingi

    ReplyDelete
  3. Ni kweli maana wanaweza fanya figisu kuwa wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza wana CORONA

    ReplyDelete
  4. Wamekwenda na vikosi 2 na wachezaji 3 extra.Kama ni figisu hutaweza kuizuia.Kama walivyofanyiwa Namungo. Kwa raundi hizi wanakuwepo viongozi wa CAF kusimamia zoezi la upimaji wa Covid 19.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii ya viongozi wa CAF kusimamia nimeipenda

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic