March 27, 2021


 BAADA ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kupoteza mchezo wake uliopita kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea, kesho ina kazi ya kumenyana na Libya.

Stars ikiwa ipo kundi J ina pointi zake nne baada ya kucheza mechi tano. Inakutana na Libya ambayo ipo nafasi ya nne na ina pointi tatu baada ya kucheza mechi tano.

Kupotea kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Equatorial Guinea kumefuta matumaini ya Stars kufuzu Afcon hivyo kitacheza na Libya ambayo nayo imekwama kufuzu michuano hiyo mikubwa inayotarajiwa kuchezwa Cameroon.

Kim Poulsen, Kocha Mkuu wa Stars amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao huo na wana amini watapata ushindi.

"Kupoteza mchezo wetu uliopita ni somo kwani hatukuhitaji kupoteza kwa kuwa imetokea basi tunajipanga kwa ajili ya mchezo wetu ujao," .

Poulsen amerithi mikoba ya Etiene Ndayiragije ambaye alifutwa kazi kwa makubaliano kati yake na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic