January 13, 2020


MICHUANO ya kombe la mapinduzi inafikia tamati leo huko visiwani Zanzibar ikikutanisha timu mbili kutokea Tanzania bara ambazo ni Simba ya jijini Dar, na Mtibwa Sugar yenye maskani yake mkoani Morogoro, michuano hii ambayo inatimiza miaka 16 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004 hufanyika kila mwaka ili kuenzi tukio la Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika Jan 12, mwaka 1964.
Toka kuanzishwa kwa michuano hii mwaka 2004 rekodi mbalimbali zimeandikwa baadhi ya rekodi za kibabe kuwahi kuandikwa katika historia ya miaka 16 ya michuano hii tangu kuanzishwa kwake hizi hapa :-
Yanga awa bingwa wa kwanza wa michuano
Yanga kutokea mitaa ya Jangwani ndiyo timu ya kwanza kutwaa taji la michuano hii mwaka 2004 na walifanya hivyo baada ya kuifunga timu ya Mtibwa Sugar kwa magoli 2-1 yaliyofungwa na Salum Swedi na Gulla Joshua huku lile la kufutia machozi la Mtibwa likifungwa na Abubakar Mkangwa.
Azam FC baba lao
Klabu ya soka ya Azam ndiyo timu ambayo imechukua ubingwa wa mapinduzi mara nyingi zaidi kuliko klabu nyingine yoyote ikiwa imefanya hivyo mara tano ambapo mwaka 2012 iliifunga timu ya Jamhuri kutoka Pemba kwa magoli 3-1, mwaka 2013 ikaifunga Tusker ya Kenya kwa mabao 2-1, mwaka 2017 ikarudi tena fainali na kuichapa timu ya Simba kwa goli 1-0, mwaka 2018 ikaichapa URA ya Uganda kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya dakika tisini mchezo kuisha suluhu ya 0-0, na mwaka 2019 wakaja kuifunga Simba kwa magoli 2-1 na hivyo kutimiza makombe matano ya kombe hilo.
Nane wametwaa ubingwa
Toka kuanzishwa kwa michuano hii ni timu nane tu ambazo zimewahi kuchukua ubingwa wa mashindano hayo timu hizo ni; Yanga, JKU, Malindi, Simba, Mtibwa, Azam, KCCA, URA.
Ni Azam tena
Rekodi nyingine kali ya Azam katika kombe la Mapinduzi ni ile ya kutwaa ubingwa huo mfululizo ikiwa ndiyo timu pekee ambayo iliweza kutetea kombe hilo ikifanya hivyo katika vipindi vitatu tofauti mwaka 2013 baada ya kuweza kulitetea taji walilotwaa 2012 na kufanya tena hivyo mwaka 2018 wakitetea kombe walilotwaa mwaka 2017 na 2019 walitetea kombe walilotwaa 2018.
KCCA wamo
Klabu ya soka ya KCCA kutoka nchini Uganda ndiyo klabu ya kwanza alikwa kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kufanikiwa kushinda Ubingwa wa kombe la Mapinduzi ikifanya hivyo mwaka 2014 baada ya kuivua ubingwa Azam katika mchezo mkali wa fainali.

Simba v Mtibwa

Leo majira ya saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan, Simba itakuwa na kibarua mbele ya Mtibwa Sugar kupambania kombe la Mapinduzi baada ya bingwa mtetezi Azam FC kutupwa nje kwenye hatua ya nusu fainali na Simba kwa penalti 3-2 baada ya dakika tisini kutoshana nguvu ya bila kufungana.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic