March 30, 2021


 TIMU ya taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, (Beach Soccer), inayonolewa na Kocha Mkuu Boniphace Pawasa leo itakuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Burundi.

Mchezo huu ni maalumu kwa ajili ya kufuzu AFCON kwa timu za Beach Soccer ambapo mechi zote mbili zitachezwa Dar.


Akizungumza na Saleh Jembe, Pawasa amesema kuwa wanachosubiri kwa sasa ni muda wa kuingia uwanjani kukamilisha kazi ambayo wameifanya kwa muda mrefu.


“Kwa sasa tunasubiri muda wa kuingia uwanjani kumaliza kazi ambayo tumeifanya kwa muda mrefu. Tupo tayari kupata matokeo na imani yetu hatutawaangusha Watanzania vijana wanaonekana wana kitu kikubwa.


“Kile ambacho ninawapa vijana wanaonekana kuelewa na kukifanyia kazi, nimewaambia kwamba wanapaswa wajiamini katika kusaka ushindi, hivyo ninawaamini katika hilo hawatakosea,” amesema.


Mchezo wa leo utachezwa katika uwanja uliopo kwenye fukwe ya Coco Beach majira ya saa 10:00 jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic