WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen wameanza maandalizi kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu AFCON.
Machi 25 wanakibarua cha kusaka ushindi
mbele ya Equatorial Guinea kwenye mchezo ambao Stars itakuwa ugenini.
Utakuwa mchezo mgumu kwa kuwa kila timu
inapeleka wachezaji uwanjani ikihitaji ushindi hapo hesabu lazima ziwe kubwa
kwa Stars.
Furaha ya mashabiki ni kuona timu inapata
ushindi na ushindi unapatikana kwa maandalizi mazuri ndani ya uwanja. Kwa
wakati ambao upo ni lazima kujipanga na kufanya kazi kwa juhudi ndani ya
uwanja.
Ikiwa wachezaji mtashindwa kujituma kwenye
kusaka ushindi itakuwa ni rahisi kwenye kukwama kufikia malengo yenu. Na
kushindwa kufikia malengo ya kupata ushindi ni pigo kwa taifa.
Mkiwa kwenye jambo la kuwakilisha nchi
kwenye mashindano ya kimataifa hapo kazi ni moja kupeperusha bendera ya
Tanzania bila kuogopa ndani ya uwanja.
Ukweli upo wazi kwamba kila mchezaji ambaye
ameitwa kuitumikia timu ya taifa upo wazi na hali hiyo imepeleka kila mmoja akapata
nafasi ya kuitwa kikosini kupambana na timu kwa ajili ya majukumu ya Tanzania.
Jambo la kuzingatia ni nidhamu na kuwa
wasikivu kwa kile ambacho mwalimu anawaambia. Ikiwa mtafuata maelekezo ya
benchi la ufundi itaongeza nguvu na ari kwa mashabiki kuendelea kuwafuatilia
kwenye mechi zenu zote.
Imani yetu ni kwamba mnaweza kufanya
makubwa ndani ya uwanja kwa kuwa uwezo mnao na hilo lipo wazi. Uwezo wenu
unapaswa utumike kwa ajili ya kupambania taifa letu ambalo linapenda kufuatilia
mpira.
Nguvu kubwa itumike katika kuelewa kile
ambacho mnafundishwa na kukifanyia kazi ndani ya uwanja. Muda wa maandalizi ni
muda pekee wa kurekebisha makosa ambayo mnayafanya ndani ya uwanja.
Hii itazidi kuwafanya mzidi kuwa sokoni kwa
kuwa kadri mnavyofanya vizuri mnazidi kuwa kwenye ramani ya kuwa sokoni hasa
kwa wale ambao wanawafuatilia.
Wachezaji pambaneni bila kuchoka ndani ya
uwanja ili kuweza kufanya vizuri. Ushindani upo wazi ndani ya uwanja nanyi pia
ongezeni juhudi katika kusaka matokeo.
Jambo kubwa la kufanya ni kukubali
kujifunza na pale ambapo mnakosea ndani ya uwanja mna kazi ya kurkebishana
wenyewe kwa wenyewe ili kusaka matokeo kwenye mechi zenu ambazo mtacheza.
Kila mchezaji anapenda kuona timu inapata
matokeo mazuri. Ikiwa morali itakuwa kubwa kwa kila mchezaji itaongeza nguvu
pia ya kupata matokeo mazuri wakati ujao kwenye mechi za ushindani.
Ikumbukwe kwamba wakati timu ikiwa Kenya mchezo wa kwanza wa kirafiki ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.
Mchezo wa pili ulifutwa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kwa sababu ya kifo cha Rais wa awamu ya tani, John Magufuli ikiwa ni sehemu ya maombolezo kwa shujaa ambaye alikuwa ni mpenda michezo.
Imani yangu ni kwamba wachezaji mtazidi
kupambana kwa ajili ya mechi zote za ushindani kitaifa na kimataifa. Kikubwa ni
kuongeza juhudi na kufanya kazi kwa kujituma ndani ya uwanja.
Ligi pia kwa sasa ipo kwenye mzunguko wa
presha ambapo kila timu imekuwa ikihaha kufikia malengo yake ndani ya uwanja.
Msimu huu tunaona kwamba umekuwa ni wa
tofauti kidogo kwa namna kasi yake inavyokwenda ni muhimu kuweza kujifunza kwa
ajili ya yale makosa ambayo yanatokea ndani ya uwanja.
Kwa kufanya vizuri kwa wachezaji kwenye
mechi hizi ni fursa ya kuweza kupata nafasi kwenye timu ya Taifa Stars kwa kuwa
mwalimu amekuwa akifuatilia na rekodi kwa timu husika na nyingene amekuwa akipewa.
Makosa ambayo yemekuwa yakiripotiwa ni
muhimu kufanyiwa kazi kwa kuwa jambo la msingi ni kuona kwamba timu inapata
matokeo chanya bila makelele yoyote ndani ya uwanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment