MOHAMED Hussein, ’Zimbwe’ nahodha msaidizi wa Klabu ya Simba bao lake mbele ya Al Merrikh limeweka rekodi Afrika kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kufunga katika hatua ya makundi ndani ya kikosi hicho.
Chini ya Didier Gomes, Simba inayoongoza kundi A na pointi 10,
imefunga jumla ya mabao matano manne yote yalifungwa na wageni hivyo bao lake
limeweka rekodi kwa msimu wa 2020/21.
Mabao hayo ya Simba yalifungwa na Chris Mugalu mwenye mabao
mawili, mbele ya AS Vita na Al Merrikh yeye ni raia wa Congo, Luis Miquissone
ana mabao mawili alifunga mbele ya Al Ahly na Al Merrikh.
Bao la kwanza la mzawa ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Simba limefungwa na Zimbwe, Uwanja wa Mkapa yeye ni beki wa kushoto chaguo namba moja
la Gomes.







Aongeze juhudi
ReplyDeleteKaza but zimbwe usilewe sifa
ReplyDeleteSema mtanzania kwa timu ya simba.ukizngumzia kiujumla kmbka kna msuva wa waydad alishafnga goli pia ktk makundi
ReplyDeleteSema mtanzania kwa timu ya simba.ukizngumzia kiujumla kmbka kna msuva wa waydad alishafnga goli pia ktk makundi
ReplyDeleteDogo anajua na anajituma sana. Hongera sana kwake
ReplyDelete